🔥 Burn Fat Fast. Discover How! 💪

DIRISHA LA KUTUMA MAOMBI KADA YA AFYA LAFUNGULIWA Sifa za Mwo | Տchool PVH

DIRISHA LA KUTUMA MAOMBI KADA YA AFYA LAFUNGULIWA

Sifa za Mwombaji
Awe raia wa Tanzania
Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi Umri wa miaka 45
Awe hajawahi kuajiriwa Serikalini na kupata cheki namba na endapo mwombaji atakuwa alishaajiriwa Serikalini na kupata Cheki Namba, atatakiwa kuzingatia Utaratibu wa uhamisho au kurejea katika Utumishi wa Umma baada ya kuacha kazi kama ilivyobainishwa kwenye Waraka Na. CCB.228/271/01 wa tarehe 07 Agosti, 2012.
Mwombaji awe na sifa na weledi kwa Mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba. 1 wa mwaka 2009 kuhusu kada zilizo chini ya Wizara ya Afya kama zilivyoainishwa hapo juu.
@schoolpvh1
             
Maombi yote yaambatishwe na nyaraka zifuatazo
Nakala ya cheti cha kuzaliwa
Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne/Sita
Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts)
Nakala ya cheti cha Usajili Kamili (Full Registration)
Waombaji waliosoma nje ya Nchi waambatanishe na Ithibati (Accreditation) kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Cheti cha Mafunzo kwa Vitendo (Internship)
Maelezo Binafsi (CV)
Picha ndogo (passport size) ya hivi karibuni
@schoolpvh1
           

Maelezo ya ziada kuzingatia

Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa watumishi. Hivyo utatakiwa kuchagua eneo ambalo ungependa kupangiwa endapo utafanikiwa kupata nafasi hiyo; Aidha, hakutakuwa na kubadilisha kituo pindi utakapopata nafasi hiyo

Nakala za Vyeti vyote vithibitishwe na Mahakama au Wakili

Waombaji wanaojitolea katika mikoa mbalimbali waambatishe barua inayomtambulisha kutoka kwa Mganga Mkuu/Mfawidhi wa Mamlaka husika.

Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao (online) kupitia mfumo wa kielektroniki unaopatikana kupitia anuani ifuatayo ajira.moh.go.tz

Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja ofisini hayatafanyiwa kazi.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 29 April, 2022 saa 9.30 Alasiri.

Kwa maelezo zaidi jinsi ya kutumia mfumo huu pakua maelezo haya
@schoolpvh1