🔥 Burn Fat Fast. Discover How! 💪

OR-TAMISEMI yawaelekeza maafisa elimu mambo manne OR-TAMISEM | Տchool PVH

OR-TAMISEMI yawaelekeza maafisa elimu mambo manne

OR-TAMISEMI

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Switbert Mkama ametoa maelekezo kwa maafisa elimu kutekeleza mambo manne muhimu ya kuyazingatia wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Dkt.Mkama ameyaelekeza hayo leo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao cha utekelezaji wa mafunzo endelevu ya walimu kazini kwa maafisa elimu taaluma wa mikoa na wakurugenzi, maafisa elimu msingi, maafisa elimu taaluma msingi na wathibiti ubora wa shule kutoka halmashauri 26.

Amesema,lengo la mpango wa mafunzo hayo ni kuwa na uratibu mzuri wa mafunzo ya walimu, uwekaji wa rasilimali kwaajili ya mafunzo, uandaaji na utekelezaji na usimamizi wa mafunzo kuanzia ngazi ya shule,vituo vya walimu na halmashauri.

Dkt.Mkama aliwaagiza maafisa hao kuimarisha usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji hususani wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).

Pia amesema, japo wamefanya jitihada kubwa za kuimarisha ujifunzaji wa KKK bado kuna wanafunzi wanamaliza darasa la pili wakiwa hawamudu stadi hizo.

Pili, amesema wakaimarishe usimamizi wa ujenzi na utunzaji wa miundombinu ya shule kwani Serikali itatumia kiasi kikubwa cha fedha katika ujenzi wa miundombinu ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule za msingi kupitia mradi wa BOOST.

Tatu, amesema kila ngazi katika halmashauri ihakiki takwimu za elimumsingi kikamilifu ili wapate takwimu sahihi na bora zinazosadifu hali iliyopo shuleni amesema watafuatilia utekelezaji wa agizo hili na endapo itabainika kuwepo kwa udanganyifu wowote au uzembe hatua zitachukuliwa kwa wahusika.

Aidha, jambo la nne, amesema kumezuka wimbi la walimu kuwarekodi wanafunzi katika matukio mbalimbali na kuwaweka mitandaoni hivyo basi anewaomba watoe elimu kwa walimu wote kutofanya kitendo hicho kwakuwa kinawadhalilisha watoto wao.

‘’Nimalizie kwa kuwashukuru wadau wote katika elimu International Rescue Committee,Children in Crossfire, na age khan foundation ambao wamewezesha kikao hiki kwa kugharamia huduma za chakula na ukumbi, niwashukuru nyote kwa kufika kushiriki katika kikao hiki na ni matumaini yangu kuwa mtatekeleza mambo yote yaliyoelekezwa kupitia kikao hiki,’’amesema
@schoolpvh1