🔥 Burn Fat Fast. Discover How! 💪

Mkurugenzi wa Shule ampiga Mzazi na kitako cha bastola baada y | Տchool PVH

Mkurugenzi wa Shule ampiga Mzazi na kitako cha bastola baada ya kuomba uhamisho wa mwanaye


Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia Mkurugenzi wa shule ya Sun Academy, Nguvu Chengula, kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi Alifa Mkwawa, ambaye ni mzazi, kwa kutumia kitako cha bastola baada ya kuombwa uhamisho wa mtoto anayesoma katika shule hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Allan Bukumbi, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 6:00 mchana maeneo ya shule hiyo iliyopo mtaa wa Mawelewele ambapo chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokana na mtuhumiwa kugoma kutoa uhamisho wa mtoto wa mlalamikaji kwa kile kinachodaiwa kuwa hajalipa ada ya mtoto huyo
Chanzo: EATV