Get Mystery Box with random crypto!

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA ASTASHAHADA YA | Տchool PVH

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA ASTASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI, MSINGI NA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU SEKONDARI (SAYANSI MIAKA MITATU) KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari (Sayansi miaka mitatu). Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha NNE wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.

SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU

Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari (sayansi miaka mitatu) ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III.

 UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
1. Wahitimu wa kidato cha nne waliohitimu kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 wanaruhusiwa kutuma maombi.
2. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kufanya maombi kielektroniki kupitia tovuti (tcm.moe.go.tz)
3. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja katika vyuo wanavyotaka kusoma na vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki.
4. Mwombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali atachagua tahasusi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi.
@schoolpvh1
5. Waombaji wa nafasi za mafunzo walio kazini wanapaswa kuwa wamehitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti, Stashahada au Shahada.
6. Walimu Kazini watapaswa kuambatisha barua ya ruhusa kutoka kwa waajiri wao;
7. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu yatatolewa kupitia “account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia 07/06/2022) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa.
@schoolpvh1

8. Barua na fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (moe.go.tz) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi.
9. Mwisho wa kutuma maombi kwa Mafunzo ya Ualimu ni tarehe 31/05/2022.   

          Tanbihi: Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu
@schoolpvh
Soma taarifa hii kupitia pdf file hili hapa chini na Vyuo vitakavyo dahili kulingana na uhitaji wako