🔥 Burn Fat Fast. Discover How! 💪

NAFASI ZA AJIRA 9800 ZA WALIMU 2022 ZATANGAZWA WAZIRI wa Nchi | Տchool PVH

NAFASI ZA AJIRA 9800 ZA WALIMU 2022 ZATANGAZWA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema ajira mpya 32,604 zinazotarajiwa kutangazwa kabla ya kufikia mwisho wa mwaka huu wa fedha, zitaigharimu serikali Sh bilioni 315 kwa mwaka.

Mhagama ametoa kauli hiyo leo Aprili 12, 2022 jijini Dodoma akizungumza kuhusu utoaji wa vibali vya ajira kwa watumishi wa umma nchini.

Amesema kati ya ajira hizo 32,604, sekta zilizopewa kipaumbele ni elimu iliyopewa nafasi12,035, afya 10,285 na sekta zingine nafasi 2,392.

Amesema katika nafasi 12,035 za sekta ya elimu, nafasi 9,800 ni kwa wa walimu wa shule za msingi na sekondari, ambapo mchakato wake utasimamiwa na TAMISEMI, ilihali nafasi 2,235 ni kwa ajili ya wahadhiri wa vyuo vikuu, vyuo vya elimu ya juu na wakufunzi wa vyuo vilivyopo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambapo mchakato utasimamiwa na taasisi husika kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Kwa upande wa sekta ya afya, Mhagama amesema imekasimiwa nafasi za ajira 10,285 zinazojumuisha nafasi 7,612 kwa ajili ya hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambapo mchakato utasimamiwa na TAMISEMI.

Amesema nafasi 1,650 kwa ajili ya watumishi wa kada za afya katika Hospitali za Kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa ambapo mchakato wake utasimamiwa na Wizara ya Afya.

Pia amezitaja nafasi 1,023 kwa ajili ya vyuo vya afya, hospitali nyingine za kimkakati na zile za Mashirika ya Dini na hiari zenye mkataba na serikali.

Mhagama pia amefafanua nafasi 2,392 zinazotarajiwa kujazwa kwenye sekta zingine za kipaumbele kuwa katika kada za kilimo nafasi za ajira ni 814, kada za mifugo nafasi 700, kada za uvuvi nafasi 204, kada za maji nafasi 261 na kada za sheria nafasi 513.

Amesema mchakato wa ajira hizo utasimamiwa na wizara husika pamoja na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Waziri amefafanunua kuwa zipo nafasi 7,792 kwa ajili ya watumishi wa kada nyingine kwenye wizara, idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa na taasisi nyingine za umma.
@schoolpvh1