Get Mystery Box with random crypto!

TAMISEMI YAOMBA KIBALI CHA KUAJIRI WALIMU WAPYA ELFU 10 Wazi | Տchool PVH

TAMISEMI YAOMBA KIBALI CHA KUAJIRI WALIMU WAPYA ELFU 10


Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa leo amewasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo amesema TAMISEMI imeomba kibali cha kuajiri Walimu wapya Elfu 10.

"Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa kuna Shule za Msingi 17,034 zenye Wanafunzi 12,033,594 wakiwemo wenye mahitaji maalum 60,825 na Shule za Sekondari 4,175 zenye Wanafunzi 2,607,142 wakiwemo wenye mahitaji maalum 11,106, jumla ya Walimu waliopo ni 258,291 wakiwemo wa Shule za Msingi 173,591 na Sekondari Walimu 84,700"

"Hadi Machi, 2022 mahitaji ya Walimu Shule za Msingi ni 274,549 kwa uwiano wa 1:60 (Mwalimu mmoja kwa Wanafunzu 60), waliopo ni 173,591 na upungufu ni 100,958 sawa na 36.77% ya mahitaji, mahitaji ya Walimu kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa Shule za Msingi ni 3,631, waliopo ni 1,517 na upungufu ni Walimu 2,143 sawa na 59.02% ya mahitaji, mahitaji ya Walimu kwa Shule za Sekondari ni 159,443 waliopo ni 84,700 na upungufu ni 74,743 sawa na 46.87%"

"Katika kukabiliana na upungufu wa walimu uliopo, TAMISEMI imeomba kibali cha kuajiri Walimu 10,000 wa Shule za Msingi na Sekondari, kati ya hao 5,000 ni kwa ajili ya Shule za Awali na Msingi na 5,000 kwa ajili ya Shule za Sekondari, hii itapunguza mahitaji ya Walimu wa Shule za Sekondari kwa asilimia 6.56 na elimu ya Awali na Msingi kwa asilimia 10.65"

@schoolpvh1