🔥 Burn Fat Fast. Discover How! 💪

Watumishi waliofukuzwa kazi kwasababu ya kughushi vyeti watape | Տchool PVH

Watumishi waliofukuzwa kazi kwasababu ya kughushi vyeti watapewa haki yao.

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwa warudishiwe michango yao tu ambayo walichangia kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo kwa PSSSF ni 5% na NSSF ni 10% ya mshahara wa Mhusika na haitahusisha malipo mengine yoyote ya ziada.

Hayo yamesemwa na leo October 26, 2022 Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na wenye ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako.

Prof. Ndalichako amesema marejesho ya michango kwa Watumishi hao yataanza kufanyika kuanzia November 01, 2022 ambapo Mtumishi atatakiwa kwenda kwa aliyekuwa Mwajiri wake akiwa na nyaraka mbalimbali ikiwemo kitambulisho, nakala za kibenki na passport size.
@schoolpvh1