2022-06-06 20:48:59
Aidha amesema matokeo yanayotarajiwa kupatikana katika utekelezaji program hiyo ni vyumba vya madarasa 12,000 kujengwa ambapo lengo ni ni kujenga vyumba vya madarasa 3000 kila mwaka kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023, shule 600 kutekeleza mpango wa shule salama, vituo vya walimu shule za msingi 800 kuwekewa vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza na utoaji wamafunzo endelevu kwa walimu, madarasa 12,000 ya awali kuboreshwa na uandikishwaji wa wanafunzi wa Elimu ya awali kuongezeka, kuimarikakwa utawala katika ngazi ya shule za msingi na kuimarika kwa ubora wa walimu katika ufundishaji kutokana na mafunzo ya walimu kazini
Wakati huohuo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mhe. David Silinde amesema serikaliimepanga kuwajengea uwezo Makatibu Tawala wa Mkoa, Maafisa elimu Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa elimu wa Halmashauri, Maafisa elimu kata, wakuu wa shule na waalimu juu ya utekelezaji wa programu ya kuimarisha ujifunzaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali na Msingi
Naye Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Charles Msonde amesema serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha inaimarisha sekta ya elimu nchini kwa kujiwekea mikakati madhubuti katika utekelezaji wa afua za elimi nchini
2.5K views17:48