2022-04-17 09:57:11
"Taratibu za uhamisho wa mwanafunzi wa elimu ya msingi anayehamia nje ya nchi"]a.) Mzazi/ Mlezi aandike barua kwenda katibu mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi (WEST) akifafanua ombi lake kwa kutoa sababu za msingi kuhusu uhamisho huo. Barua hiyo iwe ni ya kupitia kwa mwalimu mkuu, Afisa Elimu wilaya na Afisa Elimu wa mkoa husika.
b). Vitambulisho vya barua viwe:-
Kadi ya Maendeleo ya mwanafunzi wa Elimu ya Msingi anaeingia Nchini.
Barua iwe na picha ya mwanafunzi
c). Afisa wa Wizara anayehusika atamwandikia barua ya kumtambulisha nchi anakokwenda.
"Taratibu za uhamisho wa mwanafunzi wa Elimu ya Msingi anayeingia Nchini"]a). Mwanafunzi atapokelewa na WEST kwa kuonesha barua toka Wizara ya nchi anakotoka, barua hiyo isainiwe na kuwekwa muhuri na mamlaka husika.
b). Vitambulisho vya barua
Taarifa ya maendeleo ya mwanafunzi kuishia darasa alilopo.
Vivuli vya passport ya mwanafunzi na mzazi/mlezi.
Taarifa ya usajili wa mwanafunzi
Kibali cha ukazi
648 views06:57