Get Mystery Box with random crypto!

Տchool PVH

Logo of telegram channel schoolpvh1 — Տchool PVH Տ
Logo of telegram channel schoolpvh1 — Տchool PVH
Channel address: @schoolpvh1
Categories: Education
Language: English
Subscribers: 11.31K
Description from channel

The center of academic resources
📚 Primary School to teachers college
Android
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.schoolpvh
iOS
https://apps.apple.com/tz/app/school-pvh/id6445867210
📞
255747272228
255626272229

Ratings & Reviews

4.00

2 reviews

Reviews can be left only by registered users. All reviews are moderated by admins.

5 stars

1

4 stars

0

3 stars

1

2 stars

0

1 stars

0


The latest Messages 27

2022-05-01 12:45:35 ni kwenye ufundi na ujuzi hivyo ni vizuri kujiandaa. Hili tunalisema mapema ili wanafunzi watakaoomba katika kipindi hicho wajue pia katika vyuo vya ufundi kuna fursa ya kupata mikopo," amesema Prof. Mkenda.
@schoolpvh

Mhe. Mkenda ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka bilioni 464 hadi kufikia bilioni
570, kuondoa adhabu ya asilimia 10 ya wanaochelewa kurejesha mikopo na kufuta asilimia 6 ya kulinda thamani.

Aidha Waziri Mkenda ametoa wito kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu juu kutoa taarifa zote zinazotakiwa kwa ukamilifu na kwa wakati ili waweze kupata mikopo hiyo bila changamoto.

"Mkopo unatolewa kulingana na taarifa anazotoa mwombaji, ukitoa taarifa ambazo sio kamili kunakuwa na changamoto hivyo toeni taarifa kamili na Bodi itaendelea kuchakata taarifa hizo
ili wanaostahili kupata mikopo wapate," amefafanua Waziri Mkenda.
@schoolpvh
1.8K views09:45
Open / Comment
2022-05-01 12:43:49
SERIKALI KUSOMESHA CHUO KIKUU WANAFUNZI WATAKAOFANYA VIZURI KWENYE MASOMO YA SAYANSI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) amesema katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23 Wizara imetenga fedha kwa ajili ya kutoa ufadhili wa elimu ya juu (scholarships) kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika masomo ya Sayansi.
Waziri Mkenda amesema hayo Jijini
Dodoma alipokutana na Wajumbe wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo amesema ufadhili huo utatolewa kwa asilimia mia moja kwa wanafunzi wachache na watasomeshwa ndani na nje ya nchi.
Amesema lengo la Serikali ni kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya juu na kuhamasisha watoto wengi kupenda kusoma masomo ya Sayansi.
@schoolpvh

Pia ametoa agizo kwa Bodi hiyo kujipanga
ili ifikapo mwaka wa fedha 2023/24 kuanza kutoa mikopo kwa wanafunzi watakaosoma masomo ya Ufundi na ujuzi kwa ngazi ya Diploma.

"Kilio cha watu wengi kwa sasa ni ajira na sehemu ambayo ajira ni rahisi zaidi ni
1.6K views09:43
Open / Comment
2022-04-29 20:59:54
https://ajira.tamisemi.go.tz/#/authentication/register
2.1K viewsedited  17:59
Open / Comment
2022-04-29 15:37:27
2.2K views12:37
Open / Comment
2022-04-28 12:34:37
Kutuma maombi ya ajira
Kwa mara ya kwanza jisajili hapa

https://ajira.tamisemi.go.tz/#/authentication/register
1.1K viewsedited  09:34
Open / Comment
2022-04-28 10:40:50
CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION (CSEE) NOVEMBER, 2022 TIMETABLE
(17
th October – 02
th November, 2022 – 051/2 FOOD AND NUTRITION PRACTICAL)

Pdf download kupitia link hii
https://www.schoolpvh.ac.tz/2022/02/necta-2022-timetables.html?m=1
1.6K views07:40
Open / Comment
2022-04-26 21:17:24 WAZIRI MKENDA ATOA FURSA KWA WAANDISHI WA VITABU NCHINI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) amesema Wizara itatenga bajeti kwa ajili ya mtu yeyote mwenye muswada wa kuandika riwaya ambazo zitashindanishwa na muswada ambao utashinda utagharamiwa uchapishaji wake na Wizara. 
@schoolpvh1

Amesema hayo Jijini Dodoma alipokutana na wawakilishi wa Mwandishi wa Kitabu cha Hesabu kilichoandikwa kwa kutumia mitaala ya Kenya, Uganda na Tanzania, David Inzofu ambapo amesema lengo ni kuona kunakuwa na Watanzania wengi wanaojitokeza kuandika vitabu. 

Waziri Mkenda amemuagiza Kamishna wa Elimu kuhakikisha kitabu hicho kinapitiwa na wataalamu kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ili kama kuna sehemu ya kuboresha iweze kuboreshwa kwa lengo la kumsaidia mwandishi huyo ili kuongeza hamasa kwa Watanzania wengi zaidi kuandika vitabu na kuhamasisha usomaji.
@schoolpvh1

“Tunataka kusaidia waandishi ambao wanataka kuandika riwaya. Tunaposema elimu yetu tunataka iakisi mahitaji ya nchi yetu na utamaduni wetu tungependa pamoja na wanafunzi kusoma vitabu vya nje wasome pia vilivyoandikwa na Watanzania,” amesema Prof. Mkenda.
@schoolpvh1

Amesema kumekuwepo na maoni ya kutumia Kiswahili kufundishia katika siku zijazo, hivyo kunahitaji maandalizi ili kuweza kufika huko, Watanzania wenyewe waandike vitabu wawe tayari, uwezo na uzoefu wa kutafsiri vitabu vya Kiingereza kuwa vya Kiswahili.

“Tungependa kukuza Kiswahili na hii inahitaji maandalizi, hivyo lazima kuwe na vitabu vingi vya Kiswahili, huwezi kuanza kutumia lugha ya Kiswahili huku vitabu vikiwa vya Kiingereza.  Huyu mwalimu David Inzofu nafurahi kwamba ametafsiri hiki kitabu kwa Kiswahili itabidi tumsaidie ili Baraza la Kiswahili lihakiki kitabu hicho,” ameongeza Waziri Mkenda.
@schoolpvh1
@schoolink_bot
549 views18:17
Open / Comment
2022-04-26 21:12:02 MITIHANI YA KITAIFA KUSAHIHISHWA KIDITALI IFIKAPO 2025. - MAJARIBIO YAENDELEA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb) amekagua na kuridhishwa na majaribio ya Mfumo wa Kidijitali wa Usahihishaji Mitihani ya Kitaifa ya Ualimu ulioandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
@nectaresults_bot

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi na kujionea Mfumo huo unavyofanya kazi, Prof. Mkenda amesema kukamilika na kufanya kazi kwa mfumo huo kutasaidia Serikali kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika wakati wa usahihishaji wa mitihani ya kitaifa.
@schoolpvh1

Waziri huyo amesema ameridhishwa pia kuona mafunzo kwa vitendo ya wasahishaji na wakaguzi wakati wa mchakato nzima wa usahihishaji wa mitihani na wahakiki wa ubora wa usahihishaji wake.
@nectaresults_bot

"Nimeambiwa Mfumo huu wa usahishaji mitihani ya Ualimu unatarajiwa kuanza rasmi kutumika mwaka huu kwa kusahihisha mitihani ya ualimu ya vyuo vyote na mwakani utaendelea katika hatua nyingiine ya kusahihisha mitihani ya kidato cha sita na tayari waalimu na wakaguzi wameandaliwa na kupatiwa vifaa husika," amesema Waziri Mkenda. 
@schoolpvh1

Mkenda amesema mfumo huo ni wa kwanza katika Afrika na umeandaliwa na vijana wa Kitanzania ambao ni wataalamu kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ambapo amesisitiza kwamba lengo la Serikali ni kuiona NECTA inafanya shughuli zake zote kidijitali ifikapo  2025.
@nectaresults_bot

Waziri Mkenda ameongezea kuwa kwa kutumia mfumo huo Serikali itaokoa zaidi ya Shilingi bilioni 37 kila mwaka pamoja na kupunguza mlolongo mkubwa wa usahihishaji wa mitihani.
@schoolpvh1

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde amesema wametengeneza mfumo huo kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Sita na maelekezo ya Waziri ya kuona namna bora ya kuandaa mifumo ya kijiditali ambayo inaweza kutumika  katika kusahihisha mitihani pamoja na shughuli nyingine za Taasisi hiyo.
 @nectaresults_bot

Dkt. Msonde amesema kuwa wataalamu wa TEHAMA wa Baraza hilo walianza kazi ambayo imeleta matokeo ya kuanzishwa kwa mfumo huo ambayo unafanyiwa majaribio ili uweze kutumika kusahihisha mitihani ya Ualimu mwaka huu.
@schoolpvh1

"Kwa Mfumo huu tunaendelea kufikia azma ya Wizara yetu ya kuwa na mifumo ili kuendesha shughuli zote kidigitali na  kutimiza lengo  la Serikali ya Awamu ya Sita la kuwa na  uchumi wa kidigitali  na kwetu sisi tumeamua shughuli zote za mitihani kuwa za kidijitali ifikapo mwaka 2025," amefafanua Dkt. Msonde.

@schoolpvh1
@schoolink_bot
@nectaresults_bot
586 views18:12
Open / Comment
2022-04-26 19:19:15
846 views16:19
Open / Comment
2022-04-26 13:15:51
TAMISEMI UFAFANUZI
1.4K views10:15
Open / Comment