2022-08-24 11:55:49
SENSA YA WATU NA MAKAAZI 2022
MASWALI YATAKAYOULIZWA WAKUU WA KAYA
SEHEMU A: UTAMBULISHO
A01. Tafadhali nitajie idadi ya watu wote waliolala katika kaya hii usiku wa kuamkia siku ya Sensa (23 Agosti 2022)
SEHEMU B: TAARIFA ZA KIDEMOGRAFIA
B01. Orodha ya majina ya wanakaya
B02. Tafadhali nitajie majina ya watu wote waliolala katika kaya hii usiku wa kuamkia siku ya Sensa,
yaani usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne ya tarehe 23 Agosti, 2022, ukianzia na jina la Mkuu wa Kaya.
B03. Je, una uhusiano gani na Mkuu wa Kaya?
B04. Je, ni mwanamme au mwanamke?
B05. Je, una umri wa miaka mingapi?
B06. Je, ni ipi hali ya ndoa kwa hivi sasa?
B07. Tafadhali nitajie namba ya simu ya mkononi
SEHEMU C: TAARIFA YA HALI YA ULEMAVU-WATU WOTE
C01. Je, una ualbino?
C02. Je, una matatizo ya kuona hata ukiwa umevaa miwani?
C03. Je, una matatizo ya kusikia hata kama unatumia shimesikio?
C04. Je, una matatizo ya kutembea au kupanda ngazi?
C05. Je, una matatizo ya kukumbuka au kufanya kitu kwa umakini?
C06. Je, una matatizo ya kujihudumia kama vile kuoga au kuvaa nguo?
C07. Kwa Kutumia Lugha ya Kawaida: Je, una matatizo ya Kuwasiliana kwa kutumia lugha ya kawaida? kwa mfano kuelewa au kueleweka?
C08. Je, una aina nyingine ya ulemavu kati ya hizi zifuatazo?
C09. Je, ni nini chanzo cha ulemavu ulionao?
C10. Je, una kifaa cha usaidizi kwa tatizo/ulemavu ulionao?
SEHEMU D: TAARIFA ZA UHAMAJI
D01. Je, ni raia wa nchi gani?
D02. Je, ni raia wa nchi zipi?
D03. Kwa kawaida unaishi Mkoa/Nchi gani?
D04. Je, kwa kawaida huwa unashinda wapi?
D05. Je, ulizaliwa Mkoa/Nchi gani?
D06. Je, ulikuja lini kuishi katika mkoa huu/nchini Tanzania?
D07. Je, umeishi kwa muda gani katika mkoa huu/Nchini Tanzania?
D08. Je, ulikuwa unaishi wapi kabla ya kuhamia hapa?
D09. Je, ni ipi sababu kuu ya kuhamia mkoa huu/nchini Tanzania?
D10. Je, ulikuwa unaishi Mkoa/Nchi gani wakati wa Sensa ya mwaka 2012?
D11. Je, ulikuwa unaishi Mkoa/Nchi gani mwaka 2021?
SEHEMU E: TAARIFA ZA VITAMBULISHO VYA UTAIFA NA UHAI WA WAZAZI
E01. Je, una vitambulisho vifuatavyo?
A. Je, una nyaraka zifuatazo za kitaifa?
B. Je, una kitambulisho cha mjasiriamali?
C. Je, baba mzazi wa yuko hai?, Je mama mzazi wa yuko hai?
SEHEMU F: TAARIFA ZA ELIMU: WATU WENYE UMRI WA MIAKA 4 AU ZAIDI
F01. Je, unajua kusoma na kuandika katika lugha ya Kiswahili, Kiingereza, Kiswahili na Kiingereza
au lugha nyingine yoyote?
F01A. Je, unaweza kufanya hesabu rahisi za kujumlisha, kutoa, kugawanya na kuzidisha katika
shughuli zako za kila siku?
F02. Je, kwa hivi sasa unasoma, uliachia, umemaliza au hujawahi kwenda shule/skuli?
F03. Je, ni ipi ilikuwa sababu kuu ya kuacha/kutowahi kwenda shule/skuli?
F04. Je, ni kiwango gani cha elimu ulichomaliza au uliachia au unachosoma kwa sasa?
SEHEMU G: TAARIFA ZA SHUGHULI ZA KIUCHUMI: WATU WENYE UMRI WA MIAKA 5
AU ZAIDI
G01. Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, Je, ni kazi/shughuli gani kati ya zifuatazo ulitumia muda
mwingi zaidi kuifanya?
G02. Ingawa hukufanya shughuli yoyote wiki iliyopita, Je, unayo kazi ya kuajiriwa, shughuli katika
shamba lako au katika biashara yako ambayo hukufanya wiki iliyopita na unatarajia kuendelea
nayo?
G03. Je, umefanya jitihada yoyote ya kutafuta kazi au shughuli katika kipindi cha wiki nne (4)
zilizopita?
G04. Je, Kwa sasa uko tayari kuanza kazi ya malipo au aina yoyote ya biashara, kilimo au kazi yoyote
kama nafasi ikitokea?
G05. Katika shughuli kuu, Je, ulikuwa huwa unajishughulisha na nini?
G06. Je, shughuli kuu unayofanya inamilikiwa na nani?
G07. Je, ni ipi shughuli kuu ya kiuchumi katika biashara au mahali unapofanyia kazi?
G08. Je, katika kipindi cha miezi 12 iliyopita yaani kuanzia Agosti 2021 mpaka usiku wa kuamkia
siku ya Sensa, ulifanya kazi kama mchimbaji mdogo wa mchanga au madini yafuatayo?
1.5K views08:55