Get Mystery Box with random crypto!

Տchool PVH

Logo of telegram channel schoolpvh1 — Տchool PVH Տ
Logo of telegram channel schoolpvh1 — Տchool PVH
Channel address: @schoolpvh1
Categories: Education
Language: English
Subscribers: 11.31K
Description from channel

The center of academic resources
📚 Primary School to teachers college
Android
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.schoolpvh
iOS
https://apps.apple.com/tz/app/school-pvh/id6445867210
📞
255747272228
255626272229

Ratings & Reviews

4.00

2 reviews

Reviews can be left only by registered users. All reviews are moderated by admins.

5 stars

1

4 stars

0

3 stars

1

2 stars

0

1 stars

0


The latest Messages 6

2023-01-16 16:11:26 Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watu wote wanaotarajia kufanya
Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), mwaka 2023 kama Watahiniwa
wa Kujitegemea kwamba;
Kipindi cha usajili kwa Watahiniwa wa Kujitegemea kimeanza tarehe 01/01/2023
hadi 28/02/2023. Ada ya usajili ni Shilingi 50,000/= kwa Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 30,000/= kwa Mtihani wa Maarifa (QT). Aidha, watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01/03/2023 hadi 31/03/2023 watalipa Shilingi 65,000/= kwa ajili ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 40,000/= kwa ajili ya Mtihani wa Maarifa (QT) ikiwa ni ada ya kawaida pamoja na faini.
@schoolpvh1
966 viewsedited  13:11
Open / Comment
2023-01-15 19:46:18 UGAWAJI VISHKWAMBI KWA WALIMU WA ZANZIBAR
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Wizara ya Elimu Bara na ile ya Zanzibar zinafanya kazi kwa kushirikiana katika suala la mageuzi ya Sera ya Elimu na maboresho ya mitaala ili kuwawezesha vijana wa pande zote mbili kupata ujuzi na stadi zitakazowasaidia kujiari ama kuajiriwa na kuchangia katika uchumi wa Taifa.
Akizungumza mjini Zanzibar Januari 11, 2023 katika hafla ya ugawaji wa vishkwambi kwa walimu wa Zanzibar vilivyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema mapendekezo yatakayopendekezwa na Serikali yatashabihiana isipokuwa tu pale ambapo mazingira yatahitaji kuwe na tofauti.
"Kuhusu suala la mageuzi ya elimu naamini hakutakuwa na tofauti kubwa kati ya Elimu ya Bara na ya Visiwani kwa kuwa kazi ya mapitio ya Sera na mitaala imefanywa kwa ushirikiano wa pande zote mbili" ameelezea Prof. Mkenda.
Kuhusu ugawaji wa Vishikwambi, Prof. Mkenda amesema Serikali imetoa vishkwambi 6,600 kwa walimu upande wa zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kugawa vishkwambi kwa walimu wote nchini katika kutambua umuhimu wa TEHAMA kwenye ufundishaji na ujifunzaji. 
Waziri huyo amesema kitendo cha Rais Mwinyi kutoa motisha ya kompyuta kwa wanafunzi waliofanya vizuri  kitachochea juhudi za wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao na hivyo kuwa tayari kujenga Taifa.
Mkenda ameongeza kuwa baadhi ya wanafunzi waliopata kompyuta wa kidato cha sita ambao walifaulu vizuri masomo ya sayansi ni wanufaika wa "Samia Scholarship" hivyo watasomeshwa bure na Serikali kupitia mpango huo.
Katika hafla hiyo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi amegawa vishkwambi kwa walimu na kompyuta mpakato kwa wanafunzi  waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa ya kidato cha nne na sita kutoka skuli za Zanzibar katika kuwapa motisha wanafunzi kuendelea kufanya vizuri.
Dkt. Hussein Mwinyi amesema Serikali yake itaendelea kuipa kipaumbele cha kwanza Sekta ya Elimu kwa kuwa maendeleo yoyote hayawezi kupatikana bila ya Elimu.
Mwinyi ameongeza kuwa anaamini vishkwambi hivyo vitasaidia kupiga hatua kwenye suala zima la TEHAMA katika sekta ya Elimu.
"Ili nchi iwe na wataalamu ni lazima iwekeze kwa kiasi kikubwa kwenye elimu hivyo tutajipanga kutoa mafunzo kwa walimu waliopo na kuongeza wengine ili tuzalishe wataalamu watakaoiinua nchi," amesema Rais Mwinyi.
Kwa upande wake Mhe. Lela Mohamed Mussa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ameshukuru kwa kupokea vishkwambi hivyo 6,600 na kwamba vitagawiwa kwa Walimu wa shule za Msingi na Sekondari za umma ili wavitumie kama zana za kufundishia na kujifunzia.

@schoolpvh1
396 views16:46
Open / Comment
2023-01-15 18:58:10 Orodha ya pili ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza

Form one second selection
Tamisemi yatoa majina Kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa marudio kuingia kidato cha kwanza 2023
@schoolpvh
513 viewsedited  15:58
Open / Comment
2023-01-14 18:52:04 Mkanganyiko uliojitokeza kuhusu lugha ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi wa shule za sekondari
@schoolpvh1
638 viewsedited  15:52
Open / Comment
2023-01-14 18:43:11 t.me/pvh_exams
657 views15:43
Open / Comment
2023-01-14 08:27:34
MARA: WANAFUNZI DARASA LA 7 WABAINIKA KUTOWAFAHAMU RAIS WA ZANZIBAR, WAZIRI MKUU

RC Meja Jenerali Suleiman Mzee amesema “Nimezunguka Shule tatu nimepata mmoja tu ndio mjanja nikampa Tsh. 10,000. Mtoto wa Darasa la Saba ambaye Mwaka huu anafanya Mtihani kuingia kidato cha kwanza lakini hana historia ya Nchi yetu, inaumiza, hii ni aibu.”

Soma https://jamii.app/RCMara
743 viewsedited  05:27
Open / Comment
2023-01-07 12:10:13 Masharti ya kurudia mtihani kwa shule za Sekondari

Maombi yote ya marudio ya darasa ya wanafunzi wa kidato cha 4 na 6 yapelekwe kwa Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ili yaidhinishwe ambapo maombi ya marudio ya darasa ya kidato cha 1 – 3 na 5 yapelekwe kwa Afisa Elimu wa Mkoa. (REO) wa mkoa ambao mwanafunzi alikuwa akisoma. 

Masharti yafuatayo yanahitajika ili kupitishwa:
Barua ya ombi ya marudio ya darasa la Mwanafunzi kutoka kwa mzazi/mlezi/mwanafunzi.
Barua ya kuunga mkono kutoka kwa mkuu wa shule ya awali.
Ushahidi wa kuunga mkono ombi. Kwa mfano, barua kutoka kwa daktari inayoelezea hali ya mwanafunzi.
Matokeo ya mtihani wa kidato cha 2 iwapo tu mwanafunzi anaomba kurudia kidato cha 4.
Rekodi za Kiakademia za Mwanafunzi kutoka kwa mamlaka ya shule iliyotangulia.
Picha tatu za mwanafunzi wa pasipoti.
Source
https://www.moe.go.tz/en/article/repeat-a-class-in-secondary-schools

@schoolpvh1
696 viewsedited  09:10
Open / Comment
2023-01-06 16:07:22 PRESS FTNA-SFNA 2022 - FINAL

@schoolpvh1
143 viewsedited  13:07
Open / Comment
2023-01-06 16:03:18 Watahiniwa 539,645 kati ya 633,537 wenye matokeo waliofanya mtihani huo Novemba 2022, wamefaulu sawa na asilimia 85.18

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi aliyekuwa akitangaza matokeo hayo leo Januari 4, 2022 jijini Dar es Salaam amesema kati ya watahiniwa waliofaulu asilimia 52.5 ni wasichana.

“Kati ya watahiniwa 539,645 waliofaulu wasichana ni 283,541 sawa na 52.5 na wavulana ni 256,104 sawa na asilimia 47.5,” amesema Amasi.

Jumla ya wanafunzi 690,341 walisajiliwa kufanya mtihani Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili uliofanyika Novemba mwaka jana huku wasichana wakiwa 367,013 sawa na asilimia 53.16 na wavulana 323,328 sawa na asilimia 46.84.

Kati ya wanafunzi waliosajiliwa, wanafunzi 635,130 sawa na asilimia 92 walifanya mtihani huo wakiwemo wasichana 342,210 sawa na asilimia 93.24 na wavulana 292,920.

Amasi amesema watahiniwa 55,211 sawa asilimia 8 kati ya watahiniwa waliosajiliwa hawakufanya mtihani huo, huku wavulana wakiwa ni 30,408 sawa na asilimia 9.40.

Viwango vya ufaulu wa madaraja navyo vyashuka

Hata wakati matokeo ya ufaulu wa jumla yakishuka hali ni mbaya zaidi kwenye ufaulu wa madaraja ya masomo.

Kwa mujibu wa Necta, ni asilimia 7.65 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo wamepata daraja la kwanza. Hiyo ni sawa na kusema wanafunzi takriban nane kwa kila 100 waliofanya mtihani huo ndiyo wamepata daraja la kwanza.

“Watahiniwa 47,885 sawa na asilimia 7.65 wamefaulu kwa daraja la kwanza,” amesema Amasi.

Ufaulu wa wanafunzi waliopata daraja la kwanza umeshuka kwa asilimia 5.2 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2021 ambapo wanafunzi 75,770 sawa na asilimia 12.58 ya wanafunzi waliofanya mtihani walipata daraja hilo la dhahabu.

Watahiniwa 45,288 sawa na silimia 7.15 wamepata daraja la pili, huku watahiniwa 74,359 sawa na asilimia 11.74 wamepata daraja la tatu huku zaidi ya nusu (asilimia 58.74) ya watahiniwa wakiangukia daraja la nne.

Watahiniwa 93,892 sawa na asilimia 14.82 wameshika mkia kwenye matokeo hayo kwa kupata daraja sifuri.
155 views13:03
Open / Comment
2023-01-06 16:00:09
Idadi hiyo sawa na 14.72% ya waliofanya Mtihani Nov 2022, watalazimika kukariri Masomo ya Kidato cha 2 kutokana na kufanya vibaya kwenye Mtihani wa Upimaji na kupata Daraja 0 (#Division0)

Pia, Wanafunzi 372,113 (58.74%) licha ya kufaulu, wamevuka Darasa kwa kupata kiwango cha chini ambacho ni Daraja la 4 (#Division4).
================

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili kwa mwaka 2022 huku ufaulu ukishuka kwa asilimia 7.4 ikilinganishwa mwaka 2021.
153 viewsedited  13:00
Open / Comment